Thursday, June 28, 2012

MTANDAO WA SULEDO NA HARAKATI ZA KUZUIA UHARIBIFU WA MISITU (SUNYA,LENGATEI NA DONGO) Mtandao wa suledo ni mtandao unaounganisha kata tatu ambazo kimsingi zimekuwa kama kielelezo cha utunzaji na usimamizi wa misitu ya jamii. Kata hizo ni Sunya, Lengatei na Dongo ziliamua kuungana na kuanzisha mtandao wa SULEDO wenye jumla ya vijiji kumi. Mtandao huu umejikita katika kusimamia msitu wa jamii wenye ukubwa wa 116741ha. Ili kufanikisha jukumu hilo jamii hii imeandaa kamati maalum inayoundwa na wajumbe thelathini na tatu(watatu kutoka katika kila kijiji), Zonal Environmental Committee. Katika kikao kilichofanyika tarehe 20/5/2012 kilichokuwa na shabaha ya kuutambulisha mradi wa haki katika misitu unaotekelezwa kwa pamoja kati ya Mtandao wa Jamii wa Usimamizi wa Misitu Tanzania(MJUMITA) na Shirika la Kuhifadhi Misitu ya Asili Tanzania(TFCG), wenye lengo la kuona huduma zinazotokana na mfumo wa ikolojia wa misitu unahifadhiwa kwa manufaa ya jamii na taifa. Mratibu wa kanda ya kati – MJUMITA alitumia nafasi hiyo kuujulisha mtandao huo kuwa pamoja mambo mengine kuna fungu maalum kwaajili ya kusaidia suala la ufuatiliaji wa kesi zinazohusu uharibifu wa misitu. Akizungumzia changamoto wanazokabiliananazo wanasuledo, maneja wa hifadhi ya msitu wa suledo Alais Nangoro alisema, uvunaji haramu wa mbao ndio tatizo kubwa la hifadhi yetu, tumekamata mbao 178, na ufuatiliaji wa kesi hizo unahuitaji gharama kubwa, Tunashukuru kupitia mradi huu tutaweza kupambana na uhalifu wa msitu wetu alisisitiza
Meneja wa msitu wa jamii wa suledo(Alais Nangoro) akionyesha mbao zilizokamatwa zikiwa makao makuu ya SULEDO kijiji cha Sunya (20/5/2012) John Reuben - Mratibu kanda ya kati - MJUMITA